Posts

Showing posts from September, 2018
Image
KISANDUKU CHEUSI" KATIKA NDEGE NI HIKI (Cheusi, Ama Chekundu) Ni kawaida kila inapotokea ajali ya ndege ya abiria, umma hutangaziwa kuwa kinatafutwa Kisanduku Cheusi; je, hicho ni nini? Hakika hicho si sanduku la kawaida, ila ni kifaa cha ndege kinachofanana na sanduku, lakini pia kutokana na udogo wake kuliko sanduku la kawaida ndio maana huitwa kisanduku. Ili kuweza kukifahamu vyema kifaa hicho, ngoja twende taratibu tuangalie jinsi kinavyofanyakazi kwenye ndege, vipimo vyake, kilibuniwa lini, gharama yake na huwekwa sehemu gani kwenye ndege. Pia, tutaangalia kwa uchache baadhi ya matukio ya ajali ambayo kifaa hicho kiliweza kusaidia kutanzua utata ambao uliibuka wakati wa uchunguzi wa ajali husika. Sababu za kufanya chunguzi hizo ni kujaribu kubaini chanzo cha kutokea ajali, na hivyo kuondoa dhana mbalimbali ambazo huibuka kuhusiana na tukio lenyewe. Lakini pia tafiti hizo husaidia waundaji wa ndege kuchukua hatua kurekebisha kasoro (kama zipo), hususan k...