Bofya hapa kuona. MBUNGE APAGAWA NA KASI YA MAGU. Bonyeza hapo juu.
Posts
Showing posts from April, 2019
DAKIKA 30 JINSI MAREKANI ILIVYOFANIKISHA KUMUUA OSAMA BIN LADEN
- Get link
- X
- Other Apps
Mwaka 2001, mwezi Desemba katika milima ya Tora Bora baada ya mapambano ya siku kumi na moja toka tarehe 6 hadi 17 na mabomu kadhaa kudondoshwa katika milima hiyo hatimaye askari wa miguu walianza zoezi la kuikagua milima hiyo kuangalia kama kuna masalia yoyote muhimu yanayoweza kuwapa fununu ya kuielewa vita waliyoianzisha kati yao Majeshi ya Marekani na Wanamgambo wa Taliban. Katika mchakato huo wa ukaguzi wanajeshi wa marekani walifanikiwa kumuokota kijana mmoja wa umri wa mika 21 akiwa hai. Baada ya kumuokota wanajeshi kadhaa wakampakia katika chopa ya kivita na kurudi nae katika kambi ya kijeshi ya Bagram Air Base iliyo nchini Afghanistan. Baada ya kufika katika kambi ya Bagram wanajeshi wakaanza kumuhoji kijana huyo ajieleze yeye ni nani na alikuwa anafanya nini katika milima ya Tora Bora. Baada ya kujitambulisha kijana huyo akawaeleza kuwa alikuwa anawinda katika milima hiyo ya Tora Bora na kwa bahati mbaya akajikuta ameingia kwenye eneo ambalo hakujua kuwa kulikuwa na mapig...