Mauaji yanayoendelea ya CHADEMA
> John Mnyika: Katika hali ya kawaida tungeweza kutoa tamko la kulaani mauji ya viongozi wetu na wafuasi wa CHADEMA lakini inachoonekana kulaani peke yake haitoshi. Serikali haitilii maanani mauji haya na kwanini yatokee kwa CHADEMA tu? katika hali hii ya sasa ya kufululiza kuuwawa kwa viongozi wetu wa CHADEMA, inaonekana sisi ndio walengwa. Sasa tunatoa wito kwa wanachama wetu na viongozi wa CHADEMA tuchukue tahadhari sana mana hawa watu wamedhamiria kutumaliza . ==>> John Mnyika :Msajili wa Vyama vya Siasa alitutaka tuandike barua kujibu yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo Kinondoni kwa kile kinachoitwa tumevunja sheria na sisi tumemjibu mengi. Msajili anasukumwa na Rais Magufuli - ==>>John Mnyika : Msajili wa vyama vya siasa anasukumwa , dhamira yao ni kutafuta mwanya wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jambo hili hawaliwezi na kama wanafikiri wanauwezo wa kuifuta CHADEMA wajaribu kufanya hivyo. Wafahamu kwamba wakizuia mlango wa demokrasia, watu wa...