
> John Mnyika: Katika hali ya kawaida tungeweza kutoa tamko la kulaani mauji ya viongozi wetu na wafuasi wa CHADEMA lakini inachoonekana kulaani peke yake haitoshi. Serikali haitilii maanani mauji haya na kwanini yatokee kwa CHADEMA tu?
katika hali hii ya sasa ya kufululiza kuuwawa kwa viongozi wetu wa CHADEMA, inaonekana sisi ndio walengwa. Sasa tunatoa wito kwa wanachama wetu na viongozi wa CHADEMA tuchukue tahadhari sana mana hawa watu wamedhamiria kutumaliza .
==>> John Mnyika :Msajili wa Vyama vya Siasa alitutaka tuandike barua kujibu yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo Kinondoni kwa kile kinachoitwa tumevunja sheria na sisi tumemjibu mengi. Msajili anasukumwa na Rais Magufuli -
==>>John Mnyika : Msajili wa vyama vya siasa anasukumwa , dhamira yao ni kutafuta mwanya wa kukifuta Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jambo hili hawaliwezi na kama wanafikiri wanauwezo wa kuifuta CHADEMA wajaribu kufanya hivyo. Wafahamu kwamba wakizuia mlango wa demokrasia, watu watafanya siasa kwa njia nyingine, sisi tutakabiliana na msajili kwa njia yoyote kuhakikisha jambo hili halifanikiwi"
==>> John Mnyika :unashangazwa na ukimya wa Msajili wa Vyama vya Siasa kwenye haya matukio ya kuuawa kwa wanachama wetu. Yeye ndio mlezi wa vyama hivi, tulitarajia aseme kitu lakini kakaa kimya. Ina maana kwamba haoni?
==>> John Mnyika:Tunawaomba wadau wa Haki za Binadamu wafuatile watu takribani watatu waliopigwa risasi wako mahabusu na wamenyimwa dhamana hali zao ni mbaya na Polisi hawajawapa matibabu. Hivi huu ni ubinadamu? Wanafurahi kuona hawa majeruhi wanaolalamika maumivu.
==>>John Mnyika :Kuhusu kufungua kesi juu ya unyama wanaotufanyia hadi sasa wanatuzungusha. Muda huu mawakili wetu wamekaa mahakamani kuhakikisha kesi hii inafunguliwa leo na tunajua huu ni mchezo tu wanatuchezea.
==>> John Mnyika:Mashirika ya Kimataifa yanapaswa kufahamu kuwa Tanzania hivi sasa kuna mauaji ya kisiasa na tunawaambia watanzania hivi sasa hali ilipofikia msikubali kuwafungulia mlango usiku wa manane watu hata kama wanajitambulisha ni askari
Comments
Post a Comment