NAMNA YA KUTUMIA BIDHAA ZENYE HYDROQUINONE KWA USAHIHI

FAHAMU MATUMIZI SAHIHI KWA BIDHAA ZENYE HYDROQUINE. Kutokana na vipodozi vingi vya kung'arisha,kupendezesha,kuvutia,kuondoa chunusi,kuondoa mafuta na mambo mengine ya kiurembo kuwekwa kiambata sumu "HYDROQUINONE" tutaangalizia namna sahihi ya kutumia ili kupunguza madhara yake kwenye ngozi na afya kwa ujumla. Hydroquinone ni kiambata kinachowekwa katika bidhaa za ulembo ili kuweusha,kung'arisha na kuondoa chunusi na madoa katika ngozi hasa usoni. kujua vipodozi hivyo bofyahttps://www.blogger.com/blog/post/edit/5639560547725395238/1499525389980259265 SERIKALI kupitia mamlaka zake zinazuia matumizi ya bidhaa zenye Hydroquinone kutokana na madhara yake kwenye ngozi na afya kiujumla. Adora Ezeonu ni mwanamke wa Nigeria amesema " Unapopanga bajeti ya wiki au mwezi,lazima uhusishe hela ya kununua mafuta au sabuni hizi,ni bidhaa muhimu kama ilivyo kwa sabuni,nguo na mambo mengine kama umeme na maji. Aliendelea kusema" Nilizaliwa na ngozi nyeusi ambayo ilinifanya nionekane mbaya na nisio na mvuto. Nilijisemea nikimaliza shule na kupata kazi nitanunua ili niwe mweupe na kuonekana mrembo zaidi. Zimenisaidia vizuri sana hadi sasa na nimeolewa na mwanaume mzuri na ninafuraha sasa. Sijaona sababu ya watu kuona matumizi ya vipodozi hivi kama ni shida ya kisiasa. Taarifa za karibuni za Shirika la Afya Duniani(WHO) imeonyesha taifa la Nigeria linaongoza kwa matumizi ya Hydroquinone kwa Afrika(77%), ikifuatiwa na Togo 59%, Afrika Kusini 35%, Senegal 27% na Mali 25%. Kongo ndio taifa lenye watumiaji zaidi wa kiume kwa bara la Afrika. ATHARI ZA HYDROQUINONE. Ukiachilia mbali madhara ya kikemikali kama cancer na kuungua kwa ngozi, Hydroquinone imeonekana imewaathiri wanawake wengi sana huko Senegal,Mali na Niger. Sura zao zimekuwa nyekundu sana,tofauti na matarajio yao ya kuwa weupe. SABABU ZA KUGEUKA KUWA NGOZI NYEKUNDU Wataamu wa vipodozi na urembo wameeleza sababu ya ngozi kuwa nyekundi ni kutokan na kuchomwa na jua kali la mchana. Inaelezwa Hydroquinone inamadhara sana kama mtumiaji atakuwa juani hasa jua la kuanzia saa 5 hadi saa 8. Hii inatokana na watumiaji wengi wanatumia bidhaa hizi kujipodoa zaidi asubuhi na kwenda kushinda juani kutwa mzima. Pia kwa wakazi wanaoishi maeneo ya joto kali inawaletea matokeo hasi zaidi kulinganisha na wanaoishi maeneo yasio na joto kali. MATUMIZI SAHIHI YA HYDROQUINONE NI JIONI. Kwakuwa madhara mengi yanasababishwa na jua,hivyo mtumiaji lazima ahakikishe wakati wa jua kali(mchana)hatumii mafuta au bidhaa hizi. Inashauriwa kutumia bidhaa hizi wakati wa jioni baada ya kuoga na ukiamka asubuhi nawa au oga na usipake tena mafuta haya au usipake chochote. Hii itakuwa umetumia vipodozi hivi bila ya kuwakiwa na jua kali hivyo kuleta matokeo mazuri na kupunguza athari za ngozi na afya kwa ujumla. JE,KUNA BIDHAA ZA KUNG'ARISHA NGOZI ZISIZO NA HYDROQUINONE? Ndio zipo na ni za asili(natural) na ni nzuri sana kwa matumizi ya binadamu. Like na share Page yetu Starlick Premium kujifunza zaidi. Hairuhusiwi kukopi na kupesti bila ya kutaja chanzo hiki. Mada ijayo MAFUTA YA KUNG'ARISHA YASIO NA MADHARA(YASIO NA HYDROQUINONE) (Picha za hapo chini ni matokeo ya matumizi ya Hydroquinone, kushoto kabla na kulia ni baada ya matumizi).

Comments

Popular posts from this blog

NAMBA ZA POLISI TANZANIA

Namtumbo District

VIPODOZI HATARI NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI