Asalaam alaykum Ama kwa mara ya kwanza naandika haya humu kwa sababu tu yamenigusa na hii wenyewe waambiwe tu ili wajue. Katika sakata la uuzaji wa shule za Umoja wa Wazazi Tz serikalini, zinazoshindwa kujiendesha lilishindikana kwa sababu (kuu)ni kwa kuwa umoja huu ulianzishwa kwa ajiri ya elimu sasa kama wataziuza maana yake umoja wa wazazi utakufa.Pia kwa kuwa wanaweza kuzifufua basi wasishindwe mapema hivi. Sababu hizi na zingine nyingi zilipuuzia mbali makubaliano ya kikao cha kamati utekelezaji makao makuu ambao walikubali kuziuza shule zote zenye wanafunzi chini ya 100. Katika kuondoa wazo la uuzaji shule basi wakuu wote wa shule hizi waliitwa Dodoma ili kupewa semina na maelekezo na taarifa. Baadhi ya maelekezo ni kuhakikisha ndani ya miezi sita kuanzia mwezi huo basi lazima shule iwe na wanafunzi zaidi ya 100, sera ya ulipaji mishahara ya walimu itapitiwa upya, mkuu wa shuke marufuku kutoa mkataba kwa mwalimu au mtumishi yeyoye,ajira zote makao makuu na maagizo mengi yalitoka....
Comments
Post a Comment