Drugs(vidonge vye kemikali) vya weza kubadilisha mwili na uwezo wa kufikilia
Kila siku unatumia vitu vingi kama chakula katika mwili wa binadamu.Unameza chakula, maji na kuvuta hewa(kupumua). Hata hivyo baadhi ya vitu ukila vinaweza pelekea kubadili hali ya mwili katika utendaji kazi, vitu ambavyo vinapelekea kubadili hali ya mwili kufanya kazi au kuhisi vinaitwa dragi(Drug)
Dragi ambayo watu wanatumia kutibu hali flani ya matatizo ya kiafya inaitwa Dawa (Medicine). Dawa zote ni dragi lakini baadhi ya dragi sio Dawa.
Kuna aina nyingi sana za madawa baadhi zinadungwa mwilini kwa njia ya sindano,baadhi zinafyonzwa na ngozi(absorbed by skin),zingine zinatumiwa kwa kunywa, zingine kwa njia ya kumeza na baadhi kwa kunusa na kupaka
Watu wengi wanasaidiwa na hizi dawa lakini baadhi wanaathiriwa kwa matumizi mabaya ya hizi dawa.Dragi ikitumika vizuri basi inaitwa dawa lakini ikitumika vibaya tunaita matumizi haramu ya dawa(dawa za kulevya) au drug abuse.
Madawa ya kulevya ni dragi ambazo hutumiwa vibaya na watu bila ya kuwa na tatizo la kiafya na mara nyingi haifuatwi masharti ya dragi hizo(na mtumiaji). Kwa hiyo kutumia dawa bila ya sababu na bila kufuata masharti tunaita, Matumizi mabaya ya dawa, (dawa za kulevya).
Matumizi ya madawa ya kulevya yanapotumiwa mara kwa mara hupelekea kwa hali ya Utegemezi wa madawa ya kulevya. Utegemezi wa dawa za kulevya(drug dependence ni mahita ya kihisia au kimwili kutumia dawa.
Comments
Post a Comment