VIPODOZI HATARI NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI
VIPODOZI VYENYE SUMU NA VISIVYO SALAMA KWA MATUMIZI/ VILIVYOZUILIWA
......................................... SEHEMU YA KWANZA 1.0 UTANGULIZI
Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au
zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza
kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na
vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji. Hivyo hujumuisha : -Vipodozi ambavyo
havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA) -Vipodozi vyenye
viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na
dawa Tanzania (TFDA) -Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha -Vipodozi
ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi) -Vipodozi ambavyo
maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza Vinaweza vikawa ni
mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika. 1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA
SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo
kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni
lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:
Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine) Steroids (Mifano ni
Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)
Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo Chloroform Bithionol
Hexachlorophene Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo Vinyl chloride
Zirconium na kemikali zinazotokana nayo Methyelene chloride Halogenated
salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)
Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants) 1.2 JINSI YA KUJUA KAMA
KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU Angalia kwenye
lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno
jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna
kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka
12. Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi
chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula
na dawa Tanzania (TFDA). Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako
kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa
kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani.
Ambalo pia ni kosa kisheria. Mifano Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY.
Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku. Losheni/krimu
ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa
matumizi na zimepigwa marufuku Krimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE
DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina
viambata Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku
SEHEMU YA PILI 2.0 MADHARA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA Vipodozi visivyo salama
vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi
madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni. Pia vipodozi hivi vina
athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia
matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na: -Ugonjwa wa
saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na
kibofu cha mkojo -Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo -Magonjwa ya
moyo na kutopumua vizuri -Kutokwa na chunusi kubwa kubwa -Ngozi kuungua, maumivu
makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele -Ngozi kuwa nyembamba sana na
laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa
kupona au hakitapona -Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi -Kichefuchefu,
kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu -Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu
(hasa kichwani) -Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na
waliopo tumboni -Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi
kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi -Kuchubuka kwa ngozi -Ngozi
kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali -Upofu, uziwi na upotevu wa
fahamu wa mara kwa mara -Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
2.2 USHAURI Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama
ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema
kuvijua na kuviepuka kabisa ili usiweze kupata madhara. Pili msaidie
kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi
visivyo salama Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama
acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa
(TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa Epuka kabisa vipodozi visivyo salama.
Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani. SEHEMU YA TATU 3.0 ORODHA YA
VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA Vifuatavyo ni vipodozi
visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi
hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani. 3.1 Krimu, Losheni na Jeli
zenye kiambato cha Hydroquinone Mekako Cream Rico Complexion Cream Princess
Cream Butone Cream Extra Clair Cream Mic Cream Viva Super Lemon Cream Ultra Skin
Tone Cream Fade-Out Cream Palmer’s Skin Success (Pack) Fair & White Active
Lightening Cream Fair & White Lightening Cream Fair & White Strong Bleaching
Treatment Cream Fair & White Body Clearing Milk Maxi-Tone Fade Cream Nadinola
Fade Cream Clear Essence Medicated Fade Cream Peau Claire Body Lotion Reine
Clair Rico Super Body Lotion Immediate Claire Maxi –Beauty Lotion Tura Lotion
Lkb Medicated Cream Crusader Skin Toning Cream Tura Bright & Even Cream Claire
Cream Miki Beauty Cream Peau Claire Crème Eclaircissante Sivoclair Lightening
Body Lotion Extra Clair Lightening Body Lotion Precieux Treatment Beauty Lotion
Clear Essence Skin Beautifying Milk Tura Skin Toning Cream Madonna Medicated
Beauty Cream Mrembo Medicated Beauty Cream Shirley Cream Kiss – Medicated Beauty
Cream Uno21 Cream Princess Patra Luxury Complexion Cream Envi Skin Toner Zarina
Medicated Skin Lightener Ambi Special Complexion Lolane Cream Glotone Complexion
Cream Nindola Cream Tonight Night Beauty Cream Fulani Cream Eclaircissante Clere
Lemon Cream Clere Extra Cream Binti Jambo Cream Malaika Medicated Beauty Cream
Dera Heart With Hydroquinone Cream Nish Medicated Cream Island Beauty Skin Fade
Cream Malibu Medicated Cream Care Plus Fairness Cream Topiclear Cream Carekako
Medicated Cream Body Clear Cream A3 Skin Lightening Cream Ambi American Formula
Dream Successful Symba Crème Skin Lite ‘N’ Smooth Cleartone Skin Toning Cream
Ambi Extra Complexion Cream For Men Cleartone Extra Skin Toning Cream O’nyi Skin
Crème A3 Triple Action Cream Pearlight Elegance Skin Lightening Clere Cream
Clear Touch Cream Crusader Ultra Brand Cream Ultime Skin Lightening Cream Rico
Skin Tone Cream Baraka Skin Lightening Cream Fairlady Skin Lightening Cream
Immediate Claire Lightening Body Cream Jaribu Skin Lightening Lotion Amira Skin
Lightening Lotion A3 Clear Touch Complexion Lotion A3 Lemon Skin Lightening
Lotion Kiss Lotion Princess Lotion Clear Touch Lotion Super Max-Tone Lotion No
Mark Cream Body Clear Top Clear Ultra Clear Peau Claire Lightening Body Oil G &G
Dynamiclair Lotion G & G Teint Uniforme G & G Cream Lightening Beauty Cream
Dawmy – Lightening Body Lotion Maxi White Cream Bioclare Lightening Body Lotion
3.2 Vipodozi vingine vyenye Hydroquinone Fair & White Powder (Exclusive
Whitenizer & Serum) New Youth Tinted Vanishing Cream Skin Success Fade Cream
Regular Teint Clair Clear Cpmplexion Body Lotion Mareme Cream Si Clair Plus
Cream Clair & White Body Cream Body White Lotion Bio Claire Cream Forever Aloe
MSM Gel Kroyons Baby Oil 3.3 Sabuni zenye kiambato cha Hydroquinone Body Clear
Medicated Antiseptic Soap Blackstar Cherie Claire Body Beauty Lightening &
Treating Soap Immediate Claire Body Beauty Soap Lady Claire G.C Extra Clear Top
Clear Beauty Complexion Soap Ultra Clear 3.4 Vipodozi vyenye Hydroquinone pamoja
na Steroid Clear Essence Skin Beautifying Milk For Sensitive Skin Fair & White
Clarifiance Fade Cream Fair & White Exclusive Whitenizer Body Lotion Fair &
White Exclusive Whitenizer Cream Fair & White Exclusive Whitenizer Gel Fair &
White Maxitone Lightening Lotion Sun Block Fair & White So White Skin Perfect
Gel 3.5 Sabuni zenye kiambato cha Mercury (Zebaki) na michanganyo yake Movate
Soap Miki Soap Jaribu Soap Binti Jambo Soap Amira Soap Mekako Soap Rico Soap
Tura Soap Acura Soap Fair Lady Elegance Block & White Skin Whitener Germicidal
Bath Soap Rose Beauty Soap Maxi-Tone Soap (Skin Lightening Soap) Margostara Soap
(New Tannin) Rusty – Whitening Soap (New Formula) Emani Natural Fair Pearls Soap
3.6 Krimu zenye kiambato cha Mercury na michanganyiko yake Pimplex Medicated
Cream New Shirley Medicated Cream 3.7 Krimu zenye Steroids (Betamethasone,
Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, Dexamethasone nk) Amira Cream Jaribu
Cream Fair & Lovely Super Cream Neu Clear Cream Plus (Spots Remover) Age Renewal
Cream Visible Difference Cream (Neu Clear Spots Remover) Body Clear Cream Sivo
Clair Fade Cream Skin Balance Lemon Cream Peau Claire Cream Skin Success Cream M
& C Dynamic Clair Cream Skin Success Fade Cream Fairly White Cream Clear Essence
Cream Miss Caroline Cream Lemonvate Cream Movate Cream Soft & Lovely Cream
Mediven Cream Body Treatment Cream (Spots Remover) Dark & Lovely Cream Sivo
Clair Cream Musk – Clear Cream Fair & Beautiful Cream Beautiful Beginning Cream
Diproson Cream Demovate Cream Top Lemon Plus Lemon Cream Beta Lemon Cream
Tenovate Cream Unic Clear Super Cream Topifram Cream First Class Lady Cream 3.8
Vipodozi vingine vyenye kiambato cha Steroid Fashion Fair Gel Plus Hot Movate
Gel Hyprogel Mova Gel Plus Secret Gel Secret Cream Peau Claire Gel Plus Hot
Proson Gel Skin Success Gel Plus Skin Clear Gel Plus Soft & Beautiful Gel Skin
Fade Gel Plus Ultra – Gel Plus Zarina Plus Top Gel Action Demovate Gel Plus
Prosone Gel Skin Balance Gel Wrinkle Remover TCB Gel Plus Demo – Gel Plus Regge
Lemon Gel Ultimate Lady Gel Topifram Gel Plus Clai & Lovely Gel Fair & White
Serum Exclusive Whitenizer Maxi White Lightening Body Milk Maxitone Cleansing
Milk Avoderm Cream Niomre Cream Niomre Lotion Nyala Lightening Body Cream Si
Clair Cream Cute Press White Beauty Lotion White SPA Rose Lotion White SPA UV
Lightening Cream 3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku Bio
Valley Sliming Gel 3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku African Gold
Super Glo Sofn Free Hair Foodblue Cap Shampoo Marhaba Anti-Dandruff Hair Cream
Blue Cap Spray Blue Cap Cream 3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku Bio
Light Cream Salon Dermaplex Amazon Clay 9Normal To Dry Skin) Beauty Secrets Body
Cream Swiss Soft N White Lightening Gel Whitening Complex Mask 3.12 Vipodozi
Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho Eye Shadow Gel Eye Shadow
Gel 02 Eye Shadow Gel 07 Eye Shadow Gel 08 Eye Shadow Gel 09 Eye Shadow Gel 10
TAHADHARI : VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO
VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI. Mara
zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.
Comments
Post a Comment