SUMU YA MAJI, DALILI NA MADHARA YAKE

 Kila seli katika mwili inahitaji Maji ili kuweza kufanya kazi kwa ufasaha.

Hata hivyo unywaji wa maji mengi au unywaji wa maji uliopitiliza unaweza kupelekea ugonjwa wa Sumu ya Maji kitaalamu unaitwa water poisoining au water intoxication au hata kuleta madhara mengine ambayo ni hatari sana kwa afya.
Ni vigumu sana kunywa maji mengi kwa bahati mbaya au kutokufahamu,lakini hali hii inaweza ikamkuta mtu ambae amepoteza maji mengi sana mwilini hasa kwa kuvuja jasho jingi, mfano kufanya mazoezi makali au hata mafunzo ya kijeshi.
Dalili za ugonjwa huu zipo wazi mfano kuchanganyikiwa,kutapika,kichefuchefu na kizunguzungu.
Katika mazingira machache water intoxication inaweza kupelekea kuvimba au kutanuka kwa ubongo na kuhatarisha maisha kwa ujumla.
Katika makala hii tutaangalizia dalili,sababu na madhara ya unywaji maji kupitiliza na kiasi gani mtu anapaswa anywe maji.
SUMU YA MAJI WATER INTOXICATION
Water intoxication au water poisoning ni kuharibika kwa utendaji kazi wa ubongo kutokana na kunywa maji mengi sana
Kwa kunywa huko maji mengi inapelekea kuongezeka kwa maji kwenye damu. Hii inapelekea kuondoa au kupunguza kiasi cha Sodiamu kwenye damu.
Kama kiwango cha sodium kitashuka hadi kufikia chini ya 135 millimoles kwa lita bila shaka madaktari watasema unaugonjwa wa upungufu wa kemikali ya sodium kwenye damu, ugonjwa huo kitaalamu unajulikana kama HYPONATRAEMIA.

Sodium inasaidia kuweka sawa kiwango cha majimaji au ubichi ndani na nje ya seli. Wakati kiwango cha Sodium kikiwa kidogo kwa sababu za unywaji wa maji mengi, vimiminika vitatembea kutoka nje ya seli na kuingia ndani ya seli kwa wingi,hivyo itapelekea kuvimba kwa seli hizo.

HATARI YA KUNYWA MAJI MENGI HADI KUPITILIZA.
Kipindi mtu anapokunywa maji mengi na seli za ubongo kutanuka,shinikizo(pressure) itaongezeka kwenye fuvu la kichwa(skull).
Mwathirika ataanza kuona dalili zifuatazo
. Maumivu ya kichwa
. Kichefuchefu
. Kutapika.
Madhara mengine ambayo ni makubwa zaidi ni kama vile;
. Usingizi
. Kushikwa na misuri, misuri kudhoofika
. Kuongezeka kwa shinikizo la damu
. Kupumua kwa tabu n.k.

Itaendelea sehemu ya pili.

Comments

Popular posts from this blog

NAMBA ZA POLISI TANZANIA

Namtumbo District

VIPODOZI HATARI NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI