SABABU INAYOPELEKEA KUFA KWA SHULE KONGWE ZA UMOJA WA WAZAZI TANZANIA (JUMUIYA YA CCM)
Asalaam alaykum
Ama kwa mara ya kwanza naandika haya humu kwa sababu tu yamenigusa na hii wenyewe waambiwe tu ili wajue.
Katika sakata la uuzaji wa shule za Umoja wa Wazazi Tz serikalini, zinazoshindwa kujiendesha lilishindikana kwa sababu (kuu)ni kwa kuwa umoja huu ulianzishwa kwa ajiri ya elimu sasa kama wataziuza maana yake umoja wa wazazi utakufa.Pia kwa kuwa wanaweza kuzifufua basi wasishindwe mapema hivi.
Sababu hizi na zingine nyingi zilipuuzia mbali makubaliano ya kikao cha kamati utekelezaji makao makuu ambao walikubali kuziuza shule zote zenye wanafunzi chini ya 100. Katika kuondoa wazo la uuzaji shule basi wakuu wote wa shule hizi waliitwa Dodoma ili kupewa semina na maelekezo na taarifa. Baadhi ya maelekezo ni kuhakikisha ndani ya miezi sita kuanzia mwezi huo basi lazima shule iwe na wanafunzi zaidi ya 100, sera ya ulipaji mishahara ya walimu itapitiwa upya, mkuu wa shuke marufuku kutoa mkataba kwa mwalimu au mtumishi yeyoye,ajira zote makao makuu na maagizo mengi yalitoka.
Sasa katika kutimiza lengo la kutouza shule hizi mambo mengi sana yanaendelea katika SHULE za Umoja wa Wazazi. Kwa kutumia shule ya sekondari ya Namtumbo kama kielelezo naomba kueleza yafuatayo.
Shule hii namba yake ya usajiri ni 391 ilijengwa mwaka 1986 na mwaka 1985 rasmi ilianza kupokea kidato cha kwanza.
UMILIKI WA SHULE
Shule hii inajumla ya eneo la ukubwa wa hekta 49 ,inamilikiwa na UMOJA WA WAZAZI TANZANIA(Jumuiya Ya CCM). Katibu Mkuu Umoja wa Wazazi Taifa ndie maneja na mmiliki wa shule hii (na zingine zote za umoja huu wa wazazi Tanzania).
Lakini katika dhana ya kukathimisha mamlaka Katibu Mkoa umoja wa wazazi ndie bosi ambae nae katika uendeshaji anashirikiana na Katibu wilaya wazazi.
Hawa Makatibu ikumbukwe kuwa ni wanasiasa ambapo uteuzi wake sio kwa ajiri ya shule, lakini kutokana na sheria na kanuni za Umoja wa wazazi yeye ndie meneja na bosi wa shule zote Umoja wa Wazazi Tanzania katika mkoa wake. Hii inapelekea shule kuendeshwa kwa mihemko mingi ya kisiasa na pia hata maelekezo na maagizo ni mengi sana. Shule inashambuliwa na matamko toka pande zote mbili CCM wenyewe na Umoja wa wazazi japo kikanuni CCM hawahusiki na hawana mamlaka yoyote juu ya shule hizi (umoja wa wazazi tu ndio wenye mamlaka). Kutokana na hali ya nchi ilivyo kwa sasa basi kila mtu kwa kuwa anakofia ya njano au kijani basi anasema lolote juu ya shule hii.
MATATIZO YALIYOPO
ukiachana na mfumo wa uendeshaji wa shule hii kisiasa lakini pia mambo yafuatayo yanaweza pelekea kuua shule,
1. SHULE IGHALIMIE UPATIKANAJI WA HATI MILKI KWA HARAKA.
Shule hii hadi leo haina hati miliki ya eneo linalomiliki toka ianzishwe mwaka 1986.Kwa sasa shule inalazimishwa ipatikanike hati miliki kwa nguvu zote bila kuzingatia kipato cha shule. Shule hii haina kipato kingine tofauti na ada inayolipwa na wanafunzi. Kwa sasa shule hii inawanafunzi 50 tu toka form one hadi four, na ada yake ni 700,000/= kwa mwaka ambapo inalipwa kwa awamu nne ili kumwezesha hata mwenye kipato kidogo kusomesha.
Shule hii inafufuliwa upya mwaka 2016 kulikuwa na wanafunzi 7 tu lakini kwa jitiada za walimu wanafunzi wanaongezeka siku hadi siku. Swali lililopo ni kuwa ukiachilia mbali kwa nn kipindi shule ikiwa na wanafunzi mamia hawakutafuta hati milki, ni kuwa hali yashule wao wenyewe hawaijui? Na kama wanajua wanachofanya kitawezekana cha kulazimishwa pesa milioni 2 zitoke shule?
2. UKARABATI WA MAJENGO
Shule hii tangu imeanzishwa licha ya ahadi mbalimbali za viongozi wa jumuiya na CCM haijawahi kufanyiwa ukarabati wa aina yoyote. Ikumbukwe shule hii ilijengwa kwa nguvu ya wananchi japo CCM wamejimilikisha tu. Shule inauchakavu wa majengo yote kuanzia madarasa hadi nyumba za walimu. Lakini kwa idadi hii hii ya wanafunzi wanataka shule ikarabati uchakavu huu jambo ambalo haliwezikani.
3. KUTOJALI SHULE NA WATUMISHI WAKE.
Viongozi wa shule hii hawathamini juhudi za watumishi na walimu wa shule, wao wanachojua ni kutafuta makosa tu lakini hawapongezi kwa kazi ngumu inayofanywa na walimu na watumishi wengine wa shule. Mfano mwaka 2015 shule ilikuwa ya kwanza kiwilaya na ya 3 kimkoa lakini waliahidi vingi sana kwa shule lakini hakuna walichokileta zaidi ya kupiga simu kuomba hela tu.
4. SHULE IJALI ZAIDI SHIDA ZA JUMUIYA NA CHAMA KULIKO WATUMISHI NA WALIMU.
Hili ni tatizo sugu, viongozi wanataka walimu wasipewe chao(japo kidogo) kisa tu labda shule eti kughalimia viongizi wa jumuiya wanaposafiri kwenda maeneo mbalimbali utafikiri hawana bajeti yao. Na wanafikili kwamba Walimu wanaweza fundisha bila kulipwa hii ni dhana potofu sana, hata wanafunzi walipofikia 7 ni kwa sababu walimu waliondoka wote kwa kuwa mkuu wa shule wa kipindi hicho alikuwa halipi walimu na alikuwa anamfurahisha katibu wake tu wa wakati huo.
5. VIONGOZI KUKOROMEA MKUU WA SHULE ASIPOJALI SHIDA BINAFSI NA ZA KIOFISI ZA UONGOZI
Hili nalo lilipelekea shule hapa ilipo yaani mkuu wa shule anatakiwa kupigania zaidi masilahi ya viongozi kuliko walimu na watumishi wake ili tu aendelee kupendwa na viongizi hao. Vinginevyo mkuu utatoka hapo bila kuchukua mda. Mkuu wa sasa anajari zaidi masilahi ya walimu wake na watumishi wake jambo linalopelekea shule kuamka tena kwa kuwa walimu wapo japo hata kwa masilahi madogo ila mda ukifika wanapata. Sasa mkuu wa sasa naamini hatachukua siku nyingi atafukuzwa na kwakuwa shule hii hakuna mwalimu mwenye mkataba kuanzia mkuu na wengine ufukuzaji hauna maelezo mengi. Mkuu wa sasa anahakikisha kwanza walimu na watumishi walichokubaliana wanapewa kabla ya mengine ya nje na yupo tayari aondolewe katika nsimamo wake huo, Mungu amjalie sana katika hili.Mkuu wa shule kabla ya huyu wa sasa aliondolewa kwa maandamano ya wanafunzi kwa kuwa walimu hawalipwi na wanaondoka, alikuwa anapendwa sana na hawa viongozi wa wilaya na mkoa kwa kuwa tu alikuwa anawapa kitu fulani.
6. KUTOTOA MIKATABA
Mwajiri ni makao makuu jumuiya ila mkuu atapendekeza tu majina.
Walimu wapo pale shuleni ni kama wanajitolea tu kwa sasa ila wanaimani yakuwa watapigania shule ili siku ya siku nao waweze kupata kitu kidogo. Lakini kutokuwepo na mkataba hii wengi inawakatisha tamaa kwa maana siku saa na dakika unafukuzwa kazi yaani siku ikipita basi wanamshukuru mungu japo nao hawakati tamaaa wana kaulimbiu isemayo "Tupo hapa Daima" ndio maana baadhi ya miezi walimu hawapati mishahara kwa kuwa fedha huwa hakuna kutokana na ulipaji mdo wa ada(wazazi kutolipa/kulipa kidogo)
7. SERA YA KUFUKUZA WANAOLIPA CHINI YA ADA ELEKEZI.
Mpango huu ni hatari sio tu kwa jamii bali hata kwa shule kwani idadi ya wanafunzi wasiolipa ada kamili ni robo tatu ya shule. sasa wakifukuzwa idadi itakayobaki itaweza kuendesha shule?
8. TRA
Hawa jamaa ni jukumu lao na shule inawajibika katika hilo. Ripoti ya CAG imeonyesha shule za CCM hazilipi kodi kwa miaka mingi. Ni kweli lakini kwa hali ya shule iliyofikia kuilazimisha shule ilipe madeni yote ya nyuma kuanzia 2015 ni kuua shule mchana mchana. Hela wanazotaka TRA ni roba ya bajeti ya nusu mhura wa shule na hizo pesa zikitoka basi walimu hawatalipwa kwa miezi 2 au 3 na wanafunzi watakosa chakula, ulipaji wenyewe wa ada ni wakusuasua ,shule inafungua baadhi ya watoto wanabeba elfu 10 kama elfu 10, wengine ahadi, sasa Hawa TRA wanaua shule kwa faida ndogo ya taifa na kuacha hasira kubwa ya taifa kwa baadae.
KULAZIMISHA MADENI YALIYOSAMEHEWA YALIPWE.
Kutokana na idadi ndogo ya wanafunzi katika shule Jumuiya ilikubali kuisamehe shule hadi pale itakapo kuwa na kipato kikubwa(idadi kubwa ya wanafunzi/watoa ada). Tangu uongozi mpya uingie unataka kulipa kwanza hela ya Ada kwa kila mwanafunzi ni 50 elfu iende makao makuu na pia kipindi chote kilichosamehewa walipe, hili ni Agizo.
DHANA YA KUFIKIRI WALIMU WALIOPO NDIO WALIOPELEKEA SHULE HALI HII YA SASA
Shule haijadhoroteshwa na walimu waliopo walioifaidi na kuileta hapa ilipo wameondoka. Walimu waliopo ndio walioinyanyua shule toka wanafunzi 7 hadi 50, viongozi saizi wanafunga ziara nyingi shule kwenda kuhoji kwa nini wanafunzi wapo wachache na kuhisi kama walimu waliopo wametoka nayo shule toka miaka ya 85.
My Take:
Shule hii inapiganiwa sana na Walimu ili inyanyuke ila wanasiasa wanataka kuitoa katika ramani, kwani viongozi wake ni makada wa kuu wa chama na hawana uwezo wa kuongoza shule zaidi tu ya kuongea kile kilichomo akilini mwake, kwani Elimu haiendani na Siasa kiuongozi na utawala
WAACHE PROPAGANDA KTK ELIMU.
Naomba watu washauri nini kifanyike kutokana na haya ILA usini-critisize kiuandishi na mpangilio wa hoja kwani mm sio mtalaamu saana ahsanteni sana,
MAGUFURI KAMA RAIS LAZIMA AJUE MATATIZO HAYA SABABU YEYE NDIE BABA LA BABA
Samaki anajikaanga kwa mafuta yake
ReplyDelete