SABABU YA MWAKINYO KUVULIWA MATAJI YOTE YA UBONDIA
Baada ya kuvuliwa ubingwa wa mabara wa WBF miezi kadhaa iliyopita, bondia namba moja nchini, Hassan Mwakinyo amevuliwa ubingwa wa Afika (ABU). Wikiendi iliyopita bondia huyo amevuliwa ubingwa wa African Boxing Union (ABU) alioutwaa Mei mwaka 2021 kwa kumchapa kwa Technical Knock Out (TKO), Maiala Antonio. Hiyo ni mara ya pili kwa Mwakinyo bondia namba moja nchini kuvuliwa ubingwa, baada ya miezi kadhaa iliyopita Shirikisho la Ngumi la Dunia (WBF) kutangaza kumvua ubingwa wa mabara aliokuwa akiushikilia tangu 2020 kablaa ya wiki iliyopita ABU kutangaza kumvua ubingwa wake. Septemba 3, 2021 Mwakinyo aliutetea ubingwa huo kwa kumchapa Julius Indongo kwa TKO, mapambano yote yakichezwa Dar es Salaam, ingawa hivi karibuni ABU imemuondoa kwenye orodha ya mabingwa wake. ABU ilimuondoa Mwakinyo kwenye orodha ya mabingwa na kumshusha hadi nafasi ya tatu ya ubora wa mabondia wake kwenye uzani wa super welter huku ikionyesha mkanda uliokuwa ukishikiliwa bondia huyo namba moja huko wazi, hauna ...