HAJI MANARA:HAKUNA ANAYETAKA KUMUUA MAKONDA LABDA AFE KWA STRESS ZAKE TU.
Haji Manara ameendelea kumnanga rafiki yake wa zamani, Paul Makonda ambaye kwasasa yupo kwenye mgogoro mzito na boss wake wa sasa, Gharib Mohammed(GSM). Manara amedai watu wengi wamekimbia nchi kwasababu ya uonevu wa Paul Makonda.
Manara amemtaka Makonda kuacha kutafuta huruma mitandaoni na sasa wanaongozwa kwa utaratibu badala ya ubabe. Pia Manara amehoji nani wa kumuua Makonda zaidi ya 'Stress' na kumtaka arudi Kolomije kwani sasa hana cheo.
Mwisho Manara amemaliza kwa kusema Makonda alilazimisha kuingia chumbani kwake kwasababu choo cha public sio hadhi yake.
Anyways huyu ndugu akiondoka sehemu au hamsini zenu zikiisha hana kifua, atayasema kwa mabaya yote mliyofanya kwa siri na dhahiri, hata GSM ajiandae siku wakienda sideways. Kwa Makonda pole sana, kuna muhenga alisema cheo ni kama koti la kuazima.


Comments
Post a Comment