SABABU YA MWAKINYO KUVULIWA MATAJI YOTE YA UBONDIA

Baada ya kuvuliwa ubingwa wa mabara wa WBF miezi kadhaa iliyopita, bondia namba moja nchini, Hassan Mwakinyo amevuliwa ubingwa wa Afika (ABU). Wikiendi iliyopita bondia huyo amevuliwa ubingwa wa African Boxing Union (ABU) alioutwaa Mei mwaka 2021 kwa kumchapa kwa Technical Knock Out (TKO), Maiala Antonio. Hiyo ni mara ya pili kwa Mwakinyo bondia namba moja nchini kuvuliwa ubingwa, baada ya miezi kadhaa iliyopita Shirikisho la Ngumi la Dunia (WBF) kutangaza kumvua ubingwa wa mabara aliokuwa akiushikilia tangu 2020 kablaa ya wiki iliyopita ABU kutangaza kumvua ubingwa wake. Septemba 3, 2021 Mwakinyo aliutetea ubingwa huo kwa kumchapa Julius Indongo kwa TKO, mapambano yote yakichezwa Dar es Salaam, ingawa hivi karibuni ABU imemuondoa kwenye orodha ya mabingwa wake. ABU ilimuondoa Mwakinyo kwenye orodha ya mabingwa na kumshusha hadi nafasi ya tatu ya ubora wa mabondia wake kwenye uzani wa super welter huku ikionyesha mkanda uliokuwa ukishikiliwa bondia huyo namba moja huko wazi, hauna bingwa. Kuvuliwa kwa taji hilo sasa kunamfanya Mwakinyo kutokuwa na mkanda wowote wa ubingwa, licha ya pointi zake kumbakisha kwenye nafasi ya 14 duniani kwenye uzani wake akiwa na nyota nne. "ABU ina kanuni na taratibu zake kwenye kutetea ubingwa wao, inapopita miezi sita bila kuutetea wanakuvua mkanda huo," alisema Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) Yahya Poli. Alisema kanuni za ABU bingwa wa mkanda wao anapaswa kuutetea ndani ya kipindi hicho, kikipita ubingwa huo unatangazwa kuwa wazi na ndivyo imekuwa kwa Mwakinyo ambaye tangu alipoutetea Septemba, 2021, imepita miezi saba sasa. Kuna tetesi kuwa bondia huyo alikataa kutetea ubingwa huo dhidi ya Brendon Thysse kwa Dola 20,000 ambayo ni zaidi ya Sh 42 milioni, japo hazijathibitishwa na Mwakinyo wala menejimenti yake. Mwakinyo alitwaa ubingwa wa ABU wa mabara Mei 2021, alipomchapa Maiala, Antonio kwa TKO, na kisha kuutetea miezi mitatu baadae yalipomchapa Julius ndongo kwa TKO. Bondia huyo ambaye yupo Nchini Marekani hivi sasa, alisema kuvuliwa ubingwa kwa kutopigana hakumuumizi sana, kwani kwake matokeo mabovu ingekuwa ni kuvuliwa ubingwa kwa kupigwa

Comments

Popular posts from this blog

NAMBA ZA POLISI TANZANIA

Namtumbo District

VIPODOZI HATARI NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU KWA MATUMIZI